ASKOFU KAKOBE AELEZA SHUHUDA ZA KUTENGENEZWA NA ZA UONGO ZA MITUME NA MANABII WA LEO ZINAVYOFANYIKA

Discussion in 'Shuhuda|Testimonies' started by Shujaa Charles CRM, Aug 29, 2019.

  1. Shujaa Charles CRM

    Shujaa Charles CRM Mtumishi level 2

    Messages:
    192
    Likes Received:
    9
    Trophy Points:
    18
    Location:
    Tanzania
    ASKOFU KAKOBE AELEZA SHUHUDA ZA KUTENGENEZWA NA ZA UONGO ZA MITUME NA MANABII WENGI WA LEO ZINAVYOFANYIKA


    Katika Siku ya Ufunguzi wa Jukwaa la Kumuhubiri Kristo (JKK) lililofanyika BCIC Mbezi Beach tarahe 18/8/2019, Askofu mkuu wa Kanisa la FGBF, Askofu Zachary Kakobe alitoa siri iliyokuwa imefichika kwa muda mrefu unaotokana na wahubiri wengi wanaohubiri juu ya maombezi na miujiza hasa kile kinachokuwa kinafanyika kwa hizi huduma za Maombezi za mitume na Manabii wa leo


    Askofu Kakobe, Alianza kwa kujipambanua kuwa anayo mamlaka ya kuzungumzia juu ya huduma hizi za maombezi na miujiza maana ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa kwanza hapa Tanzania kuanzisha huduma hizo, hivyo alieleza kuwa ana uzoefu wa muda mrefu na anafahamu, vitu vingi vya uongo na vya kutengenezwa ambavyo wahubiri wengi wa miujiza na maombezi wanavitumia na kuvifanya katika huduma hizo ili kujipatia umati wa watu wakidai Mungu ndio kawaambia au wakidai Mungu ndiye amefanya


    Askofu, huyu aliyasema hayo Baada ya kufuatwa na wachungaji na mitume na manabii ambao walimuuliza na kumueleza kuwaMBONA KUNA SHUHUDA NZURI TU ZA MAFUTA ? watu wanaenda kupaka mafuta kwenye biashara zao ,kwenye nyumba zao, nguo zao na zipo shuhuda za ajabu sana yaani mwanamke Yule alishuhudia yaani nilienda kanisani pale kila siku kuna shuhuda nyingine zinatisha?”.Walimuuliza hayo baada ya kumsikia akifundisha katika shule ya watumishi wa Mungu kupinga namna maombezi ya mafuta ya upako na maji ya upako yanavyofanyika kwa watumishi wengi wa leo kinyume na Kweli na Neno la Mungu, ndipo wakamuuliza mbona shuhuda zipo


    Sasa katika Jukwaa hilo, Askofu huyo ndio alianza kwa Kupinga na kuwashangaa watu wanaodanganyika na shuhuda wanazoziona kwenye TV na kuziona zina ukweli ndani yake.Hivyo askofu huyu alianza kutoa shuhuda moja baada ya nyingine za hivi karibuni za watumishi wa Mungu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi yetu waliokuwa wanadanganya watu wenye maTV kwa shuhuda hizo kumbe zote sio shuhuda za kweli ni za kutengenezwa na zinatokana na Wahubiri hao kutumia pesa kuwalipa watu kufanya kazi hizo ili kujipatia umaarufu na umati wa watu na pesa nyingi!!


    Yafuatayo yalikuwa ni sehemu ya mahubiri ya Askofu kakobe akielezea shuhuda moja baada ya nyingine za hao watumishi wanatumia SHUHUDA KWENYE MATV Kudanganya watu waamini ni Mungu kawambia na ni Mungu kafanya kumbe ni uongo.Fuatilia hatua kwa hatua maneno yake akielezea shuhuda hizo zilizowahumiza watu wengi na kufanya wengi kutapeliwa


    USHUHUDA WA NABII MMMOJA MAARUFU KINSHASA ALIYEKUWA ANATUMA VIJANA KUPELELEZA NA KUMPA ATAARIFA NDIPO ANATOA UNABII


    Ninyi hamjui, ninyi mnaangalia shuhuda tu kwenye Tv hizo ndio zinakubabaisha? Niulize mimi, si ndio nimeanzisha hizo shughuli.Sikiliza, mwaka 2010 nilikwenda Kinshasa(mji mkuu wa kongo DRC ) , kule tulifanya mkutano kwenye uwanja ule mkubwa, stadium kubwa kabisa kule Kinshasa inaitwa STADIDEMATEELY, Hivyo wakaja watu wakawa wanaangalia ile miujiza, kwahiyo mimi nikawa nazungumza Kiswahili na wanatafsiri Kilingala,


    Hivyo akaja mchungaji mmoja, Huyu alikuwa ni NABII MAARUFU sana, anajulikana sana Kinshasa,Akanifuata uso kwa uso akaniambia mtumishi wa Mungu hawa wote walikuwa wanashuhudia mimi nawajua, nimewaweka pembeni maana ninawafahamu hata matatizo yao, niliwai kukutana nao baadhi yao, najua hawakujui na matatizo yao nayajua ila nimeshangaa matatizo yao yametoka kwa jinsi tu unavyoomba sala fupi kwa jina la Yesu, Hii imenishangaza sana! Nitataka baadae tuzungumze .


    Siku ya mwisho wa mkutano tulizunguka makanisa karibu 10, ila tukafika kwenye kanisa hilo moja kumbe ndio hilo la NABII huyo maarufu, tulikuta watu, mamia kadhaa ya watu.Ndipo Askofu mmoja kati ya wale waliokuwa wananizunusha katika makanisa hayo sasa akaniambia


    Mtumishi nimekuleta hapa, Huyu alitaka uje kwake kwasababu alikuona kule stedium na alizungumza na wewe, lakini ni vizuri ufahamu ni nani huyu kabla ya kuzungumza nae akanionyesha uwanja ule mkubwa wa wazi, akanionyesha kuwa hawa watu unaowaona hapa kanisani kiduchu, watu waliokuwa hapa walikuwa ni wengi(Akawa ananionyesha viwanja vilee unaviona? Kule mpaka mwisho) maana watu walikuwa kama bahari, ananionyesha viwanja mpaka kule anasema WOTE WATU HAO WAMEKIMBIA ila sasa hivi ndio kama anaanza moja, na baadae huyu mwenyewe NABII akazungumza na mimi kuthibitisha hayo USO KWA USO .Ni muhimu kujua Yule Nabii ni mtu ambaye anajulikana sana kule Kinshasa maana likuwa na television yenye nguvu sana Kinshasa.Ndipo huyo akaanza kuniambia


    Huyu Nabii alikuwa mjanja muongo kwahiyo alikuwa ANASEMA ANATABIRI lakini alikuwa anatuma vijana wanaenda kusavei, kwenye nyumba alafu wanamletea habari, na kumuandikia taarifa zote juu ya nyumba hii na ile waliyoitembelea kwamba wataeleza nyumba ile namba yake,geti la kijani, kwenye geti imeandikwa kuna mbwa mkali, Yule mwanamke aliyewapokea maana walikuwa wanakaa hapo wanavizia kuangalia mwenye nyumba akiingia na kutoka na gari ambalo ni la bluu lenye namba Fulani, na Yule mwanamke ni mfupi maji ya kunde.wanachukua taarifa zote hizo, Wakigonga Hodi wanaitikiwa na yaya pale nyumbani na Yule yaya wanamuuliza jina lake anataja, wanamuulizia mama kama yupo na kupata full information na ndipo wanamletea nabii na Yule nabii anawapa pesa


    Alafu jioni kwenye kipindi chake maarufu sana ndio anazungumza huyo nabii “Hapa naona Roho ameshuka, na ananiambia kwenye nyumba hiyo hapo kwenye geti la kijani imeandikwa mbwa mkali na geti hilo kuna namba ya nyumba (anaitaja), Hapa yupo mama ambaye sijawai kukutana nae huyu mama ana gari la bluu na namba za gari (anazitaja) ana yaya wake anaitwa Fulani(anamtaja) , huyu mama ni mfupi rani yake ni ya maji ya kunde (Anataja kila kitu) , sasa wewe unayefuatilia kipindi hiki kama ni wewe ebu piga simu maana mimi sikujui na wewe jina lako unaitwa Fulani (analitaja maana jina alishapewa ) “

    Gafla baada ya maneno hayo ya nabii kwenye kipindi cha TV LIVE unasikia Simu inaita

    HUYO MAMA : HALLOOO

    NABII: HALOO : NAZUNGUMZA NA NANI?

    HUYU MAMA: “Ni mimi huyo mama uliyekuwa unanitaja, nabii yote uliyotaja ni yangu na wewe sijaonana na wewe yaani kweli Mungu ameniona eeeehe Prophet…..”


    Baada ya mazungumzo hayo anaanza kumpa na taarifa nyingine nyingine , sasa ndio anaanza kumwambia “Mungu ameniambia hivi na hivi kwa ajili yako” .Hivyo watu walikuwa wanatoa mahela kwa mahela maana mtu ulikuwa hujaonana nae na atakuuliza kuthibitisha kama mmewai kuonana au la! Hivyo watu watakuwa wanashangaa kuona amejuaje wakati hawajawai kuonana kabisa na huyo mtu.Wanaitwa “WORD OF PROPHECY (NENO LA MAARIFA)”


    Sasa kilichoteokea, maana ikaenda hivyo maana watu wengi walikuwa wanatoa hela maana wale vijana walikuwa wanatumwa kumletea habari nabii walikuwa hawaendi kwenye nyumba duni duni bali kwenye nyumba za matajiri, hivyo NI UNABII KWA WATU WENYE HELA , Kwahiyo Nabii akizungumza kwamba Mungu ananiambia ili mambo yako ya nyooke unatakiwa kutoa milioni kadhaa, hizo hela zinatoka tu kirahisi na kiwepesi


    Hivyo huyu nabii alikusanya hela nyingi, sasa wale vijana wanamleta taarifa wakamwambia hela yako imekuwa nyingi ebu tuongezee dau! Wakabishana kwenye dau, hata walipoongezewa ilikuwa ndogo sana wakadai waongezewe dau kubwa ndio kazi itaendelea, ila Yule nabii akakataa kuwaongeza dau waliyotaka ndipo mwisho hao vijana wakasema basi yatosha, wakaamua kukusanya waandishi wa habari wa vyombo vyote vizito vya Kinshasa ndipo wakaanza kuwaambia


    “Leo tumeona tuseme kweli kuhusu huyu Nabii maarufu, kwamba sisi ndio vijana wake ambao tulikuwa tunafanya nae dili, WALA HAKUNA UNABII WOWOTE UNAOTOA, hiyo ni kazi yetu maana sisi ndio tunakusanya taarifa tunamletea na yeye ndio anatamba kwenye Kipindi cha TV na kudanganya watu kuwa Eti BWANA AMENIAMBIA .Sasa hela anayokusanya ni nyingi sana kutoka kwa hao wanaowatabiria kutoka na taarifa tunazomletea hivyo sisi anatupa hela kidogo ila yeye mambo yake yamemnyookea amekuwa tajiri mkubwa lakini sisi tupo hivyo hivyo maskini, Sasa tumeona basi tukose wote


    Na wewe unayesikia huenda una dili na wahubiri Fulani hapa wanapata hela nyingi ila wewe wanakupa hela kidogo, ngoja nkikupe akili, IFIKE MAHALI NI HERI MKOSE PAMOJA NA MHUBIRI, Ebu jikusanyeni na nyinyi maana inakuwaje mnamfanyia kazi mtu mmoja anapata hela yeye wakati shughuli yote ni ya kwenu? Wakati mna uwezo wa kuikwamisha ebu shtukeni muwe na akili basi kama hawa marafiki zangu wa kinshasa!!.


    Hivyo hao vijana wakatoa ushahidi mwingi sana, wakaleta hadi wale wasichana wa kazi, mayaya walikuwa wanakutana nao magetini na kuwauliza juu ya taarifa za nyumba hizo ambazo walikuwa wanapatia taarifa za kumpelekea nabii.Hivyo ikawa ni ushahidi wa bila shaka.Hivyo hayo mahojiano ya hao vijana yote yakarushwa hivyo watu wote wakamuona Nabii amewatapeli maana alikuwa ni maarufu sana sana ,Ingawa alikuwa na hela ya kutembeza kwa mapolisi ila habari imeshaharibika ingawa hakufungwa jela kwasababu ya pesa aliyokuwa nayo ya kutoa rushwa kwa mapolisi lakini wale wote walikuwa wanakuja basi umati wote ukaondoka


    Baada ya umati mkubwa kuondoka , ndipo akasimama siku moja katika television yake mwenyewe akakiri kuwa ni kweli yaliyosemwa yote, yaani mimi natubu kwa kugaragara, AKATUBU ANALIA KWA MACHOZI huku anarusha live lakini pamoja na toba aliyofanya , watu wameumizwa bado wakaondoka ndipo wakabaki wachache.Ndipo yeye mwenyewe ananiambia baadae kuwa “Hivi vitu nilivyoviona kwako kwamba unataja tu KWA JINA LA YESU vitu vinatendeka hivi vitu Kinshasa hatuvijui, maana hivi nilivyokuwa navifanya karibu wote hapa Kinshasa ndio tunafanya hivi kwa ubabaishaji, hivyo nimetubu sana ndio hawa wachache nikabaki nao na sasa hivi ndio naanza”


    SHUHUDA WA BINTI ALIYEDAI ALIKUWA AMEVUNJIKA MIGUU KUMBE KALIPWA HELA AJIFANYE AMEPONYWA


    Namjua mama mmoja ambaye Yupo Kanisa letu FULL GOSPEL mbeya, huyu mama ana binti yake hapa Dar es salaam.Huyu mama wakati yupo mbeya akaangalia Television akamuona binti yake kwenye kipindi kimoja cha muhubiri mmoja, anatoa ushuhuda kwamba alipata ajali akavunjika miguu lakini sasa amepona, hivyo akamuona akiwa ameshika hayo magongo yake


    Sasa baada ya maombezi, akakimbia anaruka ruka , huku ametupa magongo yale na kushuhudia kuwa ameponywa.Sasa ndio Yule mama yake mdogo akampigia simu akamwambia mwanangu umepata ajali ukavunjika miguu hivyo mpaka ukatembelea magongo, mbona sisi huku mama yako wadogo hatujui wala ndugu zako wengine huko nimewauliza hawajui? Yaani kweli umevunjika miguu hujatuambia?Tunashitukia tu umetupa magongo , unatupa shock maana tunaona ushuhuda tu kwenye TV


    Ndipo Binti anamwambia mama yake mdogo, “Mama wala sijavunjika miguu, hiyo ni dili”. Binti anasema “Nilipewa Laki 3 nijifanye nimevunjika miguu, ninatembelea magongo na magongo haya ni muhubiri tu amechongesha ambayo yapo tu pale, ikiwa tu mtu akikubali anapewa tu magongo, unapigwa picha alafu unaambiwa sema hivi na vile”.Ndipo Yule Binti akamuuliza mama yake mdogo “Sasa Mama laki mitatu hapa mjini niiachie?”


    SHUHUDA ZA KUPONA UKIMWI ZA KUTENGEZWA KUTOKA NABII MKE KENYA


    ‘Hapo jirani nchi ya Kenya mwaka 2008 kulikuwapo na nabii mke (Prophetess ) jina lake anaitwa LUCY NDUTA, unaweza uka google ukaona habari zake na videos zake za youtube nyingi tu sasa huyu zilikuwa zinaoneshwa shuhuda nzito sana za watu wenye vyeti kwamba wana virusi vya UKIMWI na wameenda hospitali fulani na Manesi wanathibitisha na kushuhudia kuwa walimpokea mgonjwa kapimwa, kwahiyo vinaoneshwa vyeti vya HIV POSITIVE vya hospitali na Manesi wanashuhudia kanisani ya kwamba mtu huyo baada ya maombezi sasa mtu huyo inaonesha ni NEGATIVE mara baada ya kupimwa na vyeti vya NEGATIVE vinaoneshwa kanisani kwa wengi


    Na huyu Lucy Nduta akawa anasema kuwa dawa ya UKIMWI imepatikana kinachotakiwa ni mtu alete laki nne [400000] za kikenya na kama ilivyo laki nne za Kenya ni kama milioni nane za Kitanzania, mara moja nabii huyo Lucy Nduta atamwombea, UKIMWI utaondoka! kwa waliosikia shuhuda hizi umati ulikuwa unamiminika kwa nabii mke huyu watu walikuwa wanakanyagana,ni 2008 tu majuzi


    Sasa kilichotokea vile vitu vilikuwa vinasukwa! huyu Lucy alikuwa anakwenda kutoa hela kwa hao waliopo hospital.Anapanga anawaelekeza watu waliokwisha kuombewa wanaenda kupima wanapata hivyo vyeti vya HIV POSITIVE katika hospitali kadhaa ila kote huko watu anawapa hela hao wapimaji, anawapa hela hao manesi na wote wanaoshughulika na hospitali


    Kwa hiyo sasa, ule umati unaokuja, kumbuka laki nne za Kenya ni hela nyingi sana hivyo hela zikawa nyingi hivyo , kwahiyo wale waliokuwa wanapewa hela wakaanza kudai waongezwe kwa sababu wewe mambo yako yanakuinukia kwasababu yetu , ikawa dili limeharibika! kesi ikaenda polisi! Na ilitangazwa sana Kenya a hata uki google utaona hizo habari maana hapa ahatuzungumzi habari za kubahatisha bali tunazungumza vitu halisi vilivyopo, ukienda Nairobi ulizia juu ya Prophetess Lucy Nduta .


    Hivyo wakaleta mashahidi ,kesi ikaendeshwa muda mrefu na kesi za kule hamnaga ujanja ujanja, zikawa zinatangazwa kwenye television watu wakasikia shahidi wa watu waliokuwa wanapewa hela na dili lilivyobumbuluka , mpaka kila kitu kikawa peupe maana kulikuwa hakuna upoyaji wa aina yeyote ilikuwa watu waaandikwa wana NEGATIVE wakati watu bado wana UKIMWI na wengine baadhi yao walikufa wakati wana vyeti vya NEGATIVE


    Kufanya hadithi iwepo fupi, Kenya hakuna mchezo kama hapa Tanzania, watu wanacheza na roho za watu na kuuza uza vitu., RAIS JOHN POMBE MAGUFULI {JPM} huyu ni KAKOBE anazugumza, Ifike mahali tuwe kama Kenya , TUSIRUHUSU MATAPELI KATIKA KANISA, maana hawa ndio wanaharibu picha ya kanisa, hawa wanaharibu picha ya ukristo. Kenya alikamatwa Lucy Nduta na Polisi, kesi ikaunguruma , tunataka kusikia RAIS WETU(MAGUFULI,JPM) KWAMBA MANABII WANA KWENDA MAHAKAMANI HAPA TANZANIA.Na unajua nikisema hivi Rais John Pombe Magufuli anaisikia sauti ya Kakobe, Hivyo wewe Nabii endelea na mchezo huo UTAKAMATWA wakati wowote, utatiwa pingu wewe subiri tu


    Mkuu wetu wa mkoa,Paul Makonda Rafiki yangu, wewe umekuwa unasimama upande wa Bwana, umefanya kazi nzuri za heshima, Nakukabidhi hii kazi, KAMATA HAWA MANABII ,maana watu wanatapeliwa watu wanaumizwa kwa jina la dini, kwa jina la ukristo.Kenya walichukua hatua na taifa lile wanamuheshimu Mungu sana lakini ikawa too much, watu wanaonewa, watu waafilisiwa, Kesi iliunguruma ya Lucy nduta, na kwa taarifa yako kufanya hadithi iwe fupi ALIFUNGWA JELA MIAKA 2 na kila mtu Kenya anajua na mwaka 2010 ndipo alipofunguliwa na tangu wakati ule manabii wa Kenya wakawa makini, Ukipitiliza ukienda mbali na mstari mahakamani nenda kajieleze


    MAKALA IMEANDIKWA NA KUHARIRIWA NA:


    NA: SHUJAA CHARLES RICHARD MWAISEMBA {CRM}


    0712- 054498 / 0759- 420202

    stmwaisembac@gmail.com
     
    Frank Mushi likes this.

Share This Page