HAUONI VIZURI?: AINA YA VYAKULA VITAKAVYOBORESHA UWEZO WAKO WA KUONA

Discussion in 'Afya, Chakula na Mapishi' started by Ezekiel P Bundala, Mar 5, 2018.

  1. Ezekiel P Bundala

    Ezekiel P Bundala Unaishi kwa ajili ya Mungu na si kwa ajili yako

    Messages:
    657
    Likes Received:
    215
    Trophy Points:
    43
    Occupation:
    Pastor
    Location:
    Dodoma
    Afya ya mtu ni kitu cha kwanza kabisa katika maisha yake ya kila siku. Iwapo mtu atakosa kuwa na afya bora, au akapoteza afya yake kabisa, basi hawezi kuwa katika nafasi ya kufanya shughuli zake za kila siku sawasawa na katika ubora. Katika kitabu cha 3 Yohana 1:2, inasema kuwa, "Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako...." anaposema kwamba, na kuwa ana afya yako, maana yake mafanikio yako katika mambo yote yanategemea afya yako, bila kuwa na afya yako huwezi kufanikiwa.

    Leo nataka japo kwa ufupi nizungumze kidogo kuhusiana na afya ya macho yetu. Macho ni moja ya kiungo katika miili yetu ambacho ni muhimu sana; ni kiungo kinachotuwezesha kuona vitu katika ulimwengu huu. Pasipo macho hatuwezi kuona chochote kinachoonekana katika ulimwengu huu. Na kwa sababu macho ni kiungo muhimu sana ni lazima tuyatunze ili yazidi kuwa na afya. Macho yanapokosa kuwa na afya, uwezo wetu wa kuona vitu unapungua. Sasa nataka tuangalie aina ya vyakula ambavyo vinaweza kusaidia kuongeza uwezo wetu wa kuona. Karibu tuangalie kwa pamoja.

    1. Mboga za Majani:
    Mboga za majani zina kemikali ya luteini na zeaxanthini ambazo ni muhimu katika kulinda na kujenga uwezo wa macho kuona vizuri. Kemikali hizi hazipo tu katika mboga za majani, lakini pia zipo katika macho yako; kemikali hizi mbali ya kuwa zinajenga uwezo wako wa kuona lakini pia zinayalinda macho yako na na kiwango kikubwa cha mawimbi ya mwanga ambacho ni hatari kwa afya macho yako, kwa mfano mionzi ya ultraviolet katika mwanga wa jua.

    Watu wengi wanadhani kuwa kula mboga za majani ni umaskini, lakini ukweli ni kwamba, mboga za majani ni muhimu sana kwetu kwani zina umuhimu mkubwa sana katika afya ya miili yetu. Kwa sababu hiyo ni muhimu sana mtu ale mboga za majani kwa wingi sana, angalau katika kila mlo wake mmoja akala kiasi kidogo cha mboga za majani kuliko kutokula kabisa.

    2. Samaki:
    Samaki ni chakula bora kwa afya ya macho hasa wale wa maji baridi, kwani wamejaa asidi ya mafuta ya omega-3s (EPA and DHA) ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuzuia macho angavu (kunyauka kwa macho), kudhoofu kwa misuli ya macho na hata mtoto wa jicho. Kama umeshindwa kula vyakula hivi vya baharini unaweza kula matunda kama vile matunda damu ili kupata asidi ya mafuta ya omega-3.

    3. Nyama ya Ng'ombe
    Nyama imejaa madini ya zinki ambayo huuwezesha mwili kufyonza vitamini A ambayo ni muhimu kwa macho pia. Ikumbukwe kuwa vitamini A huuwezesha mwili kukabiliana na matatizo yatokanayo na umri au uzee.


    4. Mayai
    Mayai yana manufaa kwa ajili ya afya ya macho na miili yetu kwani yamejaa vitamini. Vitamini A inayopatikana kwenye mayai hulinda macho dhidi ya kutokuona usiku pamoja na kukauka kwa macho (macho angavu).


    5. Matunda jamii ya mchungwa na zabibu
    Matunda kama vile malimao, machenza, machungwa na zabibu yamesheheni vitamini C. Hivyo yatakuwezesha macho yako kujikinga na magonjwa kama vile mtoto wa jicho pamoja na kudhoofu kwa misuli ya macho.


    6. Karanga na jamii zake

    Vyakula hivi vimejaa mafuta ya omega-3 na vitamini E ambavyo ni muhimu kwa ajili ya afya ya macho.

    7. Matunda ya rangirangi
    Chakula kama karoti, nyanya, pilipili hoho, boga na mahindi ni vyanzo bora vya vitamini A na C. Inaaminika kuwa kemikali ya carotenoids inayoyapa matunda haya rangi zake ni muhimu kwa afya ya macho. Ikumbukwe pia vitamini C na A zina manufaa kadha wa kadha kama tulivyoona kwenye hoja zilizopita.

    8. Vyakula vya jamii ya kunde
    Vyakula vya jamii ya kunde vina kemikali kama vile Bioflavonoidi na Zinki ambavo ni muhimu kwa ajili ya ulinzi wa retina na kuzuia kudhoofu kwa misuli ya jicho.

    9. Alizeti
    Ulaji wa mbegu za alizeti utakuwezesha kupata madini ya zinki pamoja na vitamini E ambayo ni muhimu kwa ajili ya macho yako.

    Jali afya yako, tunza afya kwa gharama zote.

    Mungu akubariki sana.
     

Share This Page