LAANA ITAKAYOIPATA TANZANIA IKIRUHUSU USHOGA KUINGIA KISHERIA‼️

Discussion in 'Habari za kikristo' started by Shujaa Charles Mwaisemba, Apr 7, 2023.

 1. Shujaa Charles Mwaisemba

  Shujaa Charles Mwaisemba Mtumishi level 2

  Messages:
  178
  Likes Received:
  1
  Trophy Points:
  18
  Location:
  Tanzania
  ✳️LAANA ITAKAYOIPATA TANZANIA IKIRUHUSU USHOGA KUINGIA KISHERIA‼️

  Na:Shujaa©️®️Ⓜ️

  Kuna watu kwa kutokuelewa wanapona watu wanapaza sauti zao kupiga kelele kupinga haya maswala ya mapenzi ya jinsia moja, ya ushoga na usagaji kuingia nchini mwetu Tanzania, wanakejeli na kupuuza juhudi hizo wakidai kuwa eti tumeshachelewa kuzuia swala hilo kwani idadi ya mashoga na vitendo hivyo vimeshasambaa kote nchini

  Na zaidi wengine wanadai huwezi kuwazuia mashoga kufanya ushoga wao eti kwasababu ilishatabiriwa kwenye vitabu vitukufu kuwa hivi vitendo vitaongezeka sana nyakati hizi.Na wengine wanadai Tanzania haiwezi kushindana na mpango huu wa kimataifa wa Jumuiya ya mataifa wa kusambaza haya maswala ya mapenzi ya jinsia moja yanayokuja kwa sura ya haki za binadamu

  Kwanza,tukubaliane pamoja, kuwa tunachokipigania sio kuzuia watu kuwa mashoga maana hiyo ni tabia ya ndani ya mtu na sio kazi ya serikali kuingilia faragha za watu kinyume na sheria inavyotaka ila tunachoweza kuzuia na kupinga kama taifa ni kuzuia ushoga usiingie kwa kuhalalishwa kisheria (Legal acceptance) na kuonekana tunakubalina nalo kama wanavyofanya nchi nyinginezo. Pia na kwa kukemea hadharani pamoja na kuweka adhabu kali kwa watakaobainika kushiriki maswala haya ya ushoga kama sehemu ya kuonyesha msimamo wetu wa kulaani vitendo hivi vichafu mbele za Mungu na mbele za ulimwengu mzima

  Sisi wananchi hatupo kuwahukumu mashoga asaa maana nao wanahitaji msaaada mkubwa.Ila,kama taifa tunapaswa kuzuia mifumo yote au taasisi zozote au mashirika yeyote yanayojiendesha kwa kuonekana yanajihusisha na kuhamasisha maswala yote ya mapenzi ya jinsia moja kwa mwamvuli wa haki za binadamu

  Jambo jingine la msingi la kufahamu kwa wanachi, watawala na viongozi wengine,kuwa swala la Ushoga ni swala hatari sana sio kwa mtu tu anayefanya ushoga ila hata kwa taifa linaloruhusu na kuvumilia maswala ya ushoga mpaka kupelekea kuyaingiza na kuhalalisha kisheria kwani ni moja ya dhambi hatari zinazokaribisha sana hasira ya Mungu kuwaka kwa haraka na kumpiga sio tu mtu anayefanya ushoga bali hata nchi inayoruhusu na kuvivumilia vitendo vya kishoga na kuvihalalisha kisheria au kivitendo bila kuyachukulia hatua stahiki

  Tukumbuke, kuna adhabu au laana kubwa ambazo Mungu anazitoa kwa Taifa kama taifa pale linaporuhusu kuhalalisha machukizo kuingia katika nchi zao na wananchi pamoja na kiongozi wao wakakubaliana nalo bila kulipinga na kulikataa.Laana hizo ni kama Vimbunga,Mafuriko,Ukame,Njaa,Tufani, Magonjwa na Matetemeko n.k (YEREMIA 14:12,27:13,29:18)

  ♨️{YEREMIA 25:12} "Na itakuwa miaka hiyo sabini itakapotimia, NITAMWADHIBU MFALME WA BABELI, NA TAIFA LILE, asema BWANA, KWA SABABU YA UOVU WAO , nayo nchi ya Wakaldayo pia; nami NITAIFANYA KUWA UKIWA WA MILELE "

  Ikiwa taifa au Kiongozi wa taifa atalinyamzia au kuliruhusu jambo hili kisheria kwa kuwapa watu uhuru na haki za kuhusiana kwa kuingiliana kinyume na maumbile baina ya watu wa jinsia moja , lazima adhabu kali ya tauni, mapigo na majanga mbalimbali itashuka pia kwa nchi yetu ya Tanzania.

  ♨️{YEREMIA 34:17}
  [17]Basi BWANA asema hivi, HAMKUNISIKILIZA KUMTANGAZIA UHURU KILA MTU NDUGU YAKE, na kila mtu jirani yake; tazama, MIMI NAWATANGAZIENI UHURU , asema BWANA, yaani, wa UPANGA , NA NJAA NA TAUNI; nami nitawatoa ninyi mtupwe huko na huko katika falme zote za dunia.

  Hivyo hatupaswi kulichukulia kiwepesi wepesi maana hii dhambi ni roho kamili inayosambaa kwa haraka na yenye athari kubwa kwa taifa na ni yakupambana nayo vita kamili kiroho na hata kimwili hata ikibidi kumwagika damu WAEBRANIA 12:4

  ♨️{1 WAFALME 15:11-12}
  [11]Basi, ASA( MFALME) AKAFANYA YALIYO MEMA MACHONI PA MUNGU, kama alivyofanya babaye Daudi.
  [12]AKAWAFUKUZA MAHANITHI ( MASHOGA / SODOMITE )KATIKA NCHI, akaziondoa sanamu zote walizozifanya baba zake.

  Ni wajibu wa Rais wa Nchi kuhakikisha anafanya mema machoni pa Mungu na Ikiwa hatachukua hatua ya kulaani na kukataa ushetani huu kwa kutohalalisha kisheria haya maswala ya Ushoga ya wapenzi wa jinsia moja waliojulikana kama Mahanithi (Sodomites) itapelekea laana kubwa kwa nchi yetu

  Nguvu kubwa ya kupambana na vita hii inatokana, ikiwa watu wa Mungu watasimama katika zamu yao na kuwa wamoja kwa kuliombea Taifa kwa uzito na kumuombea Rais wa nchi yetu awe na msimamo usiotiswa na jumuiya za kimataifa kwa namna ile ile kama Mungu alivyoinusurisha Tanzania na maangamizo makubwa ya ugonjwa wa Corona ndivyo Mungu atakapolinusurisha Taifa letu na roho hii chafu kuhalalishwa nchini ili kukwepa laana na mapigo kutoka kwa Mungu

  ♨️{1 WAFALME 8:37-38}
  [37]Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao; au ukiwapo msiba wo wote, au uele wo wote;
  [38]maombi yo yote au dua yo yote ikifanywa na mtu awaye yote, au na watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu maradhi ya moyo wake, na kuikunjua mikono yake kuielekea nyumba hii;

  Tusisubiri mapigo ya Mungu kutujilia ndio tuanze kuombea Taifa letu, maana hata sasa hali ya ushoga nchini imekuwa mbaya na inatisha ila Ikiwa kama Taifa tukiomba rehema kwa Mungu na kutubu dhambi zetu na za taifa letu basi Mungu atalinusuru tena taifa letu

  Lakini pia inatupasa kupaza sauti zetu hadharani kukemea kwa kuonyesha chuki yetu dhidi ya vitendo hivi vya wapenzi wa jinsia moja kushamiri nchini, vitaipa nguvu serikali yetu ya Tanzania kuwa na msimamo na nguvu ya kusimama upande wa Mungu ya kukataa uchafu huu katikati ya ulimwengu wote uliokengeuka unaochukulia ushetani huu ni swala kawaida la haki za binadamu lakini Tanzania tunaweza kuamua kukataa hata kama tutakosa misaada kutoka nje, bali tutafurahi kwa amani na furaha aliyotupa Mungu tu

  TUSIMAME KATIKA ZAMU ZETU KULIOMBEA TAIFA LETU ILI USHOGA USIHALALISHWE KISHERIA NA KUSHAMIRI NCHINI KWA KUHARIBU JAMII YETU

  Na: Shujaa©️®️Ⓜ️

  stmwaisembac@gmail.com

  0712054498
   

Share This Page