MAMMBO 5 YA KUZINGATIA WAKATI WA KUTUMIA FIMBO. SEMINA YA MALEZI YA WATOTO! 1. Unamchapa mtoto wapi (Maeneo gani katika mwili). 2. Unamchapa mtoto na nini? (Unatumia kifaa gani kumchapia mtoto) • Usimpige mtoto kwa mikono (Kibao) • Usimpige mtoto kwa mateke. • Usimpige mtoto kwa kichwa. • Wengine hutumia gongo. • Wengine hutumia Rungu. • Wengine hutumia kisu. • Wengine hutumia mtwangio. • Wengine hutumia maji ya moto. • Wengine Kamba kuwafungia watoto kwenye miti kama adhabu. 3. Unamchapa mtoto wakati gani? • Usimchape mtoto wakati ukiwa na hasira. • Usimchape mtoto mbele ya wageni au rafiki zake jirani. • Usimchape mtoto mara kwa mara kila dakika unachapa mtoto atazoea fimbo na haitaweza kufagia tena tabia zake mbaya. • Usimchape mtoto akiwa usingizini. • Usimchape mtoto akiwa hajala yaani akiwa na njaa kali. 4. Usimchape mtoto kabla ya kumpa onyo la mdomo. • Tanguliza kwanza onyo dogo • Fuatia na onyo la kati • Onyo kali • Kisha adhabu. Mathayo 18:15 - 16 15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. 16 La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. Hatua za Biblia za kuonya mpaka kutoa adhabu: • Mtu anaonywa na mtu mmoja • Asiposikia anaonywa na watu wawili • Asiposikia anaonywa na kanisa • Asiposikia anatupiwa shetani amshughulikie. 5. Usimchape mtoto kwa kumuonea au bila kuwa na uhakika wa kosa lake. • Chunguza sababu za kumchapa mtoto kamani za hakika kabla ya kumchapa. • Usimchape mtoto kwa taarifa za kusikia tu ambazo huzazithibitisha. • Usimchape mtoto kwa kumuonea. Wakati mwingine anaweza kuwa amesingiziwa na baba au mama wa kambo. Wakati mwingine anaweza kuwa amesingiziwa na watoto wenzake ile achapwe. Wakati mwingine anaweza kuwa amesingiziwa na dada wa kazi au marafiki zake kwa sababu zao.
- Fi88 Nhà cái cá cược bóng đá, lô đề, casino uy tín nhất >>> https://bitly.com.vn/v4085p - Đánh bài online Fi88 - Game đánh bài trực tuyến - Quay hũ đổi thưởng Fi88 Cổng chơi Game Slot tiền thật