MAOMBI KWA AJILI YA KANISA LA KRISTO

Discussion in 'Maombi na Maombezi' started by Ezekiel P Bundala, May 7, 2017.

  1. Ezekiel P Bundala

    Ezekiel P Bundala Unaishi kwa ajili ya Mungu na si kwa ajili yako

    Messages:
    657
    Likes Received:
    215
    Trophy Points:
    43
    Occupation:
    Pastor
    Location:
    Dodoma
    Hakuna kipindi ambacho kanisa linahitaji nguvu ya Mungu na udhihirisho wa ishara na maajabu zinazolithibitisha Neno lake linanohubiriwa na kufundishwa kama kipindi hiki cha nyakati za mwisho katika kizazi chenye ukaidi uliokidhili. Kwa hiyo imetupasa kumwomba Mungu. Ungana na Kanisa Forum ili tuombe kwa ajili ya Kanisa la Mungu Tanzania, Afrika Mashariki, Afrika yote na duniani kote ili Mungu alijilie kanisa lake na kuleta uamsho katika nyakati hizi za mwisho.

    MAOMBI (PRAYER POINTS)

    1. Omba utakaso kwa ajili ya kanisa: Mungu alitakase kanisa lake kwa 1. Neno lake, 2. Roho wake, na 3. Kwa damu ya Yesu Kristo, ili kanisa liwe takatifu lisilokuwa na mawaa wala ila yoyote mbele za Mungu. (Yohana 17:17, 19; 1Petro 1:22; Waefeso 5:26; Waebrania 9:12, 13)
    2. Omba Roho ya kumcha Mungu iwe ndani ya kanisa; hofu ya Mungu itawale ndani ya kanisa, watu wamche Mungu, na Mungu ndiye awe hofu yao, watembee katika hofu ya Mungu ndani na nje ya kanisa. (Isaya 8:13)
    3. Omba kwa ajili ya upendo ndani ya kanisa, na umoja wa kanisa bila kujali itikadi za madhehebu. (Yohana 13:35; 1Wakorintho 12:11 - 13; 3:4 - 11; 4:6; Matendo 2:44 - 47)
    4. Omba uamsho ndani ya kanisa; Mtembeo na udhihirisho wa Roho Mtakatifu ndani ya kanisa, ibada zetu zisiwe kavu kavu, kemea roho ya mazoea, roho ya dini, roho ya kiburi na uasi, roho ya uchawi na roho ya hofu; roho zote hizi zinapingana na utendaji wa Roho Mtakatifu ndani ya kanisa. (Matendo 2:1 - 21; 2; 2Nyakati 5:11 - 14)
    5. Omba kwamba, Bwana wa mavuno apeleke watendakazi katika shamba lake; ainue Wahubiri wa Injili, Walimu wa Injili, ainue watu watakaojitoa kwa mali zao kuwapeleka wahubiri wa Injili, watakaowawezesha wahubiri kwenda, omba Mungu ainue waombezi watakaokuwa wanaomba kwa ajili ya kanisa lake na watumishi wake siku zote. (Mathayo 9:38; Luka 10:2; Isaya 59:16; Ezekieli 22:30; Isaya 63:3 - 5)
    6. Omba kwamba, kanisa la Kristo likue na kuongezeka katika kumjua Mungu hata kufikia cheo cha Kristo, lisiwe changa tena ili sisipeperushwe na kila aina ya upepo wa mafundisho ya uongo na udanganyifu. Hapa uombe pia kwa ajili ya utendaji kazi wa Huduma tano ndani ya Kanisa la Kristo; Huduma ya utume, Mungu ainue mitume; Huduma ya unabii, Mungu ainue manabii; Huduma ya uinjilisti, Mungu ainue Wainjilisti; Huduma ya uchungaji, Mungu ainue wachungaji, na huduma ya ualimu, Mungu ainue waalimu; na kwamba Mungu awajalie wote hawa kulinena Neno lake kwa ujasiri na katika uaminifu na kweli yote bila kupindisha wala kuchakachua. (Waefeso 4:11 - 16)
    Mpendwa, nyakati za mwisho zimetajwa kuwa ndio nyakati za mavuno mengi, Yesu Kristo aliwaambia wanafunzi wake, akasema, "Tazama mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno." (Yohana 4:35) Mavuno yamekwisha kuwa tayari shambani, tunachatakiwa kwanza kabisa ni KUINUA MACHO YETU TUYATAZAME MAVUNO, Mbili, TUMWOMBE MUNGU APELEKE WATENDA KAZI, Tatu, SISI KWENDA SHAMBANI ILI KUVUNA, Nne, TUOMBE KWA AJILI YA MAVUNO, Tano, TUWAPELEKE WATENDA KAZI KWA MALI ZETU. Haya yote yanaanza kwa sisi kukubali wito wa maombi, Hebu tuombe kwa ajili ya kanisa la Kristo.
     

Share This Page