MWANAMKE NA UREMBO WENYE MSINGI WAKE KATIKA TABIA NJEMA

Discussion in 'Usafi, Mapambo na Urembo' started by Ezekiel P Bundala, Apr 13, 2019.

  1. Ezekiel P Bundala

    Ezekiel P Bundala Unaishi kwa ajili ya Mungu na si kwa ajili yako

    Messages:
    657
    Likes Received:
    215
    Trophy Points:
    43
    Occupation:
    Pastor
    Location:
    Dodoma
    Urembo ni jadi ya mwanamke ye yote anayejitambua na kujua thamani yake. Ni sifa mojawapo kubwa ya mwanamke ye yote anayejitambua.

    Lakini, inawezekana wanawake wakawa hawajui urembo ni nini na nafasi yake katika maisha yao ya kila siku. Ngoja tujifunze kidogo.

    Urembo ni nini?
    Urembo ni hali ya mtu aghalabu mwanamke kuwa maridadi, nadhifu; ni ulimbwende.

    Urembo unahusisha mambo mawili;

    1. Umaridadi
    Mwanamke ili awe mrembo ni lazima awe maridadi.

    Maridadi kama nomino ni usafi aghalabu wa mavazi yote ya ndani na ya nje (yaani ya juu na ya chini).

    Maridadi kama kivumishi ni yenye kupendeza na yenye kuvutia.

    Kwa hiyo, mwanamke mrembo ni mwanamke msafi wa mavazi, mwenye kupendeza na mwenye kuvutia machoni pa watu. Hii inahusiana na MWONEKANO wake machoni pa watu katika mavazi.

    Na tunapozungumzia, ni kitu cho chote kinachovaliwa mwilini kilichotengenezwa kwa kitambaa, ngozi au plastiki kwa dhumuni la kumstiri mtu.

    Lakini pia cho chote kinachovaliwa mwilini kinachukuliwa kama vazi, hii ni pamoja na vidani vya aina zote, miwani, kofia, viatu, n.k. Vyote hivi vinakupa mwonekano fulani hivi.​

    2. Unadhifu
    Urembo ni pamoja na mwanamke kuwa nadhifu. Nadhifu ni iliyo safi na ya kupendeza; maridadi. Hii ni pamoja na usafi na mvuto wa ngozi yako kama mwanamke.​

    3. Urembo ni ulimbwende
    Ulimbwende (kwa Kiingereza "miss") ni hali ya kuwa maridadi na nadhifu katika muonekano wako wa nje, na hii inahusika na mwili wako pamoja na mavazi unayovaa.​

    Urembo haupaswi kuwa ni kitu cha kuigiza kwa sababu ni jadi ya mwanamke anayejitambua, awapo peke yake au awapo mbele za watu.

    Jadi ni nini?
    Jadi ni tabia asilia ya mtu. Ni kitu kinachotokea ndani yake, na wakati mwingine alichojifunza kutokana na malezi na makuzi katika mazingira yake aliyozaliwa na kukulia. Kwa hiyo, mwanamke anayejitambua atajizoesha kuwa mrembo au mlimbwende.

    Na kwa sababu urembo ni jadi ya mwanamke, huanzia chumbani kwake, yaani, kitandani kwake, kisha chumba kizima, lazima kiwe maridadi na nadhifu.

    Kutoka chumbani, urembo unahusisha nyumba yote, chooni, jikoni, sebuleni na katika viwanja vya nje ya nyumba anayoishi mwanamke.

    Ukitaka kumjua mwanamke mrembo, ingia chumbani kwake, kisha nenda chooni, na umalizie jikoni, kama huko hakuko vizuri, huku nje ni maigizo tu.

    UREMBO UNA MAANA KAMA KUNA SIFA NJEMA
    Sifa njema ni matokeo ya tabia njema. Na tabia njema ni tunda la ndani linaloonekana kwa nje kila penye mahusiano na watu. Ukweli ni kuwa, tabia inahusiana na namna mtu anavyoishi na kuhusiana na watu kila siku kila dakika na sekunde.

    Tabia ni chumvi katika urembo wa mwanamke. Tabia inahifadhi urembo wa mwanamke usioze na kuanza kunuka. Kama vile chumvi inavyoweza kuhifadhi samaki au vitu visiharibike, kadhalika tabia huhifadhi urembo.

    Haina maana ukawa mrembo lakini uliyekosa au uliepungukiwa tabia njema. Ni lazima uwe mwenye tabia njema ili urembo wako uwe na maana.

    Kama vile mboga isivyonoga na kupendeza kinywani isipowekewa chumvi, ndivyo urembo usivyoweza kupendeza na kuwa na mvuto machoni pa watu usipotiliwa tabia njema ya mtu huyo.

    Wakati urembo ni jadi ya mwanamke, tabia njema ni utamaduni wa mwanamke huyo ambaye ni mrembo. Kwa hiyo, mwanamke lazima awe mrembo lakini mwenye tabia njema. Wahenga walisema, uzuri wa mwanamke sio urembo ni tabia.

    Na je, Biblia inasema nini?

    1 Petro 3:3-5

    [3]Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;

    [4]bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

    [5]Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.

    Je, vipi kuhusu mavazi na urembo? Je, urembo ni lazima uzingatie namna ya uvaaji mbele za watu?

    UREMBO NA NAMNA YA UVAAJI
    Kwa wanawake wengi namna ya uvaaji ni changamoto kubwa sana hasa inapokuwa mbele za watu katika jamii zao.

    Kwa asili hakuna vazi lililo baya, au ambalo halifai kama likivaliwa mahali pake na kwa kufuata kanuni za upendo. Vazi kama vazi halina shida, ila NAMNA YA UVAAJI ndio inaweza kuwa shida na hasa kwetu sisi tulioamini. Biblia inatufundisha si aina ya mavazi ya kuvaa, bali inatufundisha namna ya kuvaa.

    Namna ya kuvaa tunayofundishwa na Biblia ni KWA KUJISITIRI; uvaaji wetu uwe uvaaji wa kusitiri miili yetu na si kuiachia wazi ionekane au kuibana ionekane.

    1 Timotheo 2:9-10
    [9]Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

    [10]bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.

    Katika maandiko haya hatuioni orodha ya mavazi ambayo tunapaswa kuvaa, ila tunaambiwa namna ya uvaaji, uwe ni wa kujisitiri pamoja na adabu nzuri.

    Adabu nzuri ni swala la tabia njema katika uvaaji wetu, ni uvaaji wenye adabu nzuri mbele za watu.

    Sasa tunaporudi kwenye urembo, ili urembo uwe na maana, kama tulivyotangulia kusema, ni lazima uwe na sifa njema. Adabu nzuri ni sifa njema, na kujisitiri ni adabu na ni sifa au tabia njema. Kwa hiyo, kuvaa lazima kuwe kwa jinsi ya kujisitiri ili urembo wetu uwe na maana.

    Urembo sio kuonyesha maungo ya mwili, si kuvaa nusu uchi, wala si kutembea uchi; urembo ni kujisitiri.

    Katika Biblia tuna mifano kabisa ya walimbwende na mmoja wao ni Esta, alivaa kwa namna ya kujisitiri na akashinda taji.

    Kuvutia, au kuwa na mvuto sio mpaka uwe uchi. Kuwa uchi kunavutia wenye matamanio ya kingono, ambao wakikuona tu fikira zao zinawapeleka kitandani wakiwa na wewe. Baada ya hapo inakuwaje sasa?

    Ni lazima wanawake mbadili mitazamo yenu; urembo si kuwavutia wanaume kingono, urembo ni kuwavutia watu wote kimwonekano wako katika adabu nzuri na kitabia kwa kuwa na sifa njema.

    Mwanamke, nirudie tena, huhitaji kuacha mwili wako nje kuwa mrembo, huo sio urembo ni uchafu na ni kukosa adabu nzuri. Unahitaji kuwa maridadi, nadhifu na mwenye tabia njema; katika kila jambo ikiwa ni pamoja na urembo ujitahidi kujipatia sifa njema kama mtu wa Mungu.

    2 Wakorintho 6:3, 4
    3 Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe;

    4 bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida;


    Na,

    Mch. Ezekiel P. Bundala
    0673184468.
     

Share This Page