*MAMBO KADHAA YA KUWEZA KUSHINDA TATIZO* *1.*Lazima Ujue Mungu ni mkubwa kuliko Tatizo. *2.*Usilitukuze Tatizo bali Mtukuze Mungu. *3.*Usilipe Tatizo Muda Mrefu wa kulitafakari bali Mtafakari Mungu kwa Muda mrefu Na utafakari uweza wake. *4.*Msifu Mungu katikati ya Tatizo lako,Maana Unapo sifu unaondoa roho ya Huzuni,ambayo ndiyo humdidimiza mtu wakati wa Tatizo. *5.*Usilifanye Tatizo liwe sehemu ya Maisha,maana Ukilifanya kuwa ni sehemu ya maisha umelipa kibali cha kudumu maishani mwako. *6.*Usikiri kshindwa bali kiri Ushindi maana Umeahidiwa ushndi kwa kila jambo. *7.*Usitazame watu wanasema nini juu ya shida yako,bali Litazame Neno la Mungu ambao ndiyo Mwamba wako ulipo simama...na Upepo(Tatizo)haliwezi kukutikisa milele. *8.*Usimweleze kila Mtu juu ya shida yako,maana wengine watakucheka,wengine hawatakuwa na chakukusaidia japo watakuonea Huruma,bali mweleze Mungu. *9.*Wakati wa Tatizo niyo wakati wa kudumu katika kutazama Ndoto za masha yako,maana lengo la Tatizo ni kukuondoa kwenye njia za ndoto zako. *10.* Mshukuru Mungu Kwa kila Jambo. Barikiweni sana tena sana na ukizingatia hyo hakika hutaona tatizo. Sent from my TECNO-Y4 using Kanisa Forum mobile app